Header Ads


 

CHUO CHA AFYA HERMAGIS CHA MOROGORO KUPUNGUZA UHABA WA WAFAMASIA NCHINI

    Kiongozi wa mbio za  Mwenye wa Uhuru Kitaifa 2021  Luteni Josephine  Mwambashi akitoa salamu na ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2021 kabla ya kuzindua Jengo la Mababara ya Chuo cha Hermagis. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Hakima Okash na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Chuo hicho Prof.Robinson Mdegela.

Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021  Luteni Josephine  Mwambashi akivuta pazia  kuashiria uzinduzi wa jengo la maabara na maabara ya Chuo cha Afya Hermags mkoani Morogoro.
Mlezi na Mshauri wa Chuo cha Afya Hermagis  Askofu Mtaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mosses akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi huo..
Mkurugenzi wa Chuo cha Afya Hermags Prof. Robinson Mdegela  akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo wa maabara uliofanywa na Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2021.
Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Afya Hermags Prof. Yonica Ngaga akieleza mikakati ya Bodi yake kwa chuo hicho pamoja na maono ya Bodi kitaaluma kwa wanafunzi mara baada ya kumaliza uzinduzi wa jengo hilo la maabara.
Meneja wa Benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro, Stephen Mapunda ambao ndio wafadhili wa shule hiyo akieleza sababu za CRDB kusaidia upanuzi wa Chuo hicho.
Kiongozi wa Mbio za  Mwenye wa Uhuru Kitaifa2021  Luteni Josephine Mwambashi akikagua maabara hiyo akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Halima Okash kabla ya kuzindua rasmi maabara hiyo.
Kiongozi wa Mbio za  Mwenye wa Uhuru Kitaifa 2021  Luteni Josephine  Mwambashi akiangalia namna Wanafunzi wa Chuo hicho wakitengenza madawa mbalimbali ikiwemo vitakasa mikono yaani SANITIZER.
Wanafunzi wa Chuo cha Hermagis wakionyesha kazi wanazozifanya chuoni hapo kwa vitendo hasa wakati wa utengenezaji wa madawa mbalimbali.

 Picha ya pamoja ya baadhi ya Wanafunzi,Wafanyakazi na viongozi wa Chuo hicho mara baada ya kuondoka kwa Mwenge wa Uhuru chuoni hapo.


Na Calvin Gwabara, Morogoro.


KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine  Mwambashi ameupongeza uongozi na Mmiliki wa Chuo Cha Afya Hermagis kwa kusaidia kuwezeshamvijana wa Kitanzania kupata Elimu ya Famasia hasa utengenezaji wa dawa na kujiajiri.

Pongezi hizo amezitoa wakati akizindua Jengo na Maabara ya kisasa  (Compound Lab) ya chuo hicho kilichopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

"Napongeza jitihada hizi kubwa zilizofanywa na wenzetu wa sekta binafsi kuanzisha chuo hiki muhimu kinachozalisha wataalamu wa famasia nchini kwetu maana mambo haya yalikuwa ya afanywa nje ya nchi ndio unaoana dawa zinaletwa nchini lakini sasa kupitia sayansi na teknolojia tunaona na sisi tuna uwezo was kuzalisha sawa hapahapa kupitia wataalamu wetu hii ni hatua kubwa na sasa nitamke kuwa mwenye wa uhuru unazindua Maabara hii" alieleza Mwambashi.

Akitoa taarifa ya Mradi huo wa ujenzi wa Maabara mkuu wa chuo hicho Benedict Lugarisha alisema kupitia maabara hiyo ya kisasa imewezesha wanafunzi kusoma kwa vitendo lakini pia kuzalisha madawa mbalimbali kama vile sabuni na vitakasa mikono yaani Sanitizer.

"Mhe. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru  Kitaifa mwaka 2021 jengo hili limeshakamilika na linavifaa vyote muhimu vinavyohitajika kwaajili ya Wanafunzi kujifunza na lina miundombinu yote muhimu hivyo tunayo heshima kubwa kukukaribisha uweze kulitembelea, kuona namna wanafunzi wetu wanavyolitumia na vifaa vyake na kisha utuzindulie jengo hili" alisema Lugarisha.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Askofu Dkt. Owdenburg Mosses amepongeza ushirikiano mkubwa ambao Serikali ya Tanzania unautoa kwa sekta binafsi katika kuanzisha Vyuo vya Afya na huduma zingine na hivyo kuwezesha kuongeza ufanisi wa wataalamu katika utoaji wa huduma.

Alisema afya ni suala nyeti na muhimu kwa maendeleo watu na taifa lolote lile Duniani hivyo chuo hicho kitasaidia kupata wataalamu wengi ambao watakwenda kusaidia jamii na taifa katika kutoa huduma sahihi za afya zinazozingatia taratibu na kanuni zinazowaongoza.

"Tunajua sote kuwa huko mtaani karibu nchi nzima kuna vyuo vingi lakini wengi wao ni wajanjawajanja tu kwenye utoaji wa taaluma kwa watoto wetu hivyo kuwepo kwa chuo chenye miundombinu bora na ushahdi tumeuona kwa wanafunzi wenyewe wanavyotengeneza madawa mbalimbali vizuri wakitoka hapa hawawezi kusubiria ajira bali wanakwenda kujiajiri wenyewe" alisema Askofu Mosses.

Mkurugenzi wa chuo hicho Prof. Robinson Mdegela ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Mvomero na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa kukubali mwenge kumulika kwenye Chuo hicho na kuahidi kuhakikisha wanaendelea kupunguza uhaba wa Wafamasia nchini hasa kutokana na umuhimu wa kada hiyo ya afya.

" Sisi hatufundishi tuu watoto kupata elimu na vyeti bali tumejikita kwenye kufundisha vya vitendo ili kila mhitimu wa Chuo chetu akitoka hapa aende kujiajiri kwenye kutengeneza madawa au akaajiriwe kwenye maeneo ambayo yana uhitaji wa Kada ya Famasia kwakuwa watakuwa wahitimu wa tofauti kutokana na Elimu bora waliyoipata hapa" alisisiza Prof. Mdegela.

Alisema kwa sasa Chuo kinatoa Mafunzo ya Famasia kwa ngazi ya Astashahada (Certificate) na  Stashahada (Diploma) kwa wanafunzi wayne ufaulu wa kuanzia alama "D" kwenye masomo ya Kemia na Baiolojia na kina mpango wa kuongeza kozi nyingine muhimu ambazo sina soko kubwa la ajira kwa wahitimu na mchango mkubwa kwa taifa.

Akielezea mikakati ya chuo hicho cha Afya Hermagis,  Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Prof. Yonica Ngaga alisema ni kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu itolewayo Chuoni hapo ili ibaki kuwa ya vitendo na kuzalisha Wahitimu watakaokuwa na mchango kwa jamii hasa kwenye sekta muhimu ya afya.

" Naomba nitumie nafasi hii kuwa shauri Wazazi, Walezi na vijana wenye sifa za kujiunga na Chuo hiki wajiunge maana hawatajutia kusoma au kumsomesha mtoto kwenye Chuo huki, Tunasomesha watoto wetu ili wapate kazi za kufanya kwa kuajiriwa au kujiajiri hivyo hapa ni mahali sahihi na mimi watoto wangu wasingekuwa wamemaliza Ngazi za juu ningewaleta hapa maana ninauhakika hatokosa kazi za kufanya" alisema Prof. Ngaga.

Alisisitiza kuwa wao kama bodi ya chuo wanataka mwanafunzi  anayetoka chuo hicho kama ni mfamasia awe na Elimu ya nadharia na vitendo na aweze kutengeneza baadhi ya dawa kwenye jamii na ajipatie fedha kupitia mtaji mdogo tu kulingana na uwezo wake au uwezo wa mzazi.

Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 unaendelea na ziara yake Mkoani Morogoro ambapo leo unepokelewa kwenye Wilaya ya Mvomero kutoka Wilaya ya Kilombero ambapo unafungua miradi mbalimbali ya maendeleo ya kusambaza ujumbe wa mwenge kitaifa kwa mwaka huu unaosema " TEHAMA ni Msingi wa Taifa endelevu, Itumie  kwa usahihi na uwajibikaji".

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.